Mahusiano nyota ya Simba na Nge ( Leo and Scorpio Compatibility)

Rakims
SIMBA NA NGE

Mtizamo unaonyesha wewe na yeye ni watu wawili tofauti sana na hamuendani kwa nafasi kubwa kwa maana wewe ni moto wa mkaa na yeye ni maji ya moto wewe ni rahisi sana kumchemsha yeye na yeye akichemka ni rahisi sana kukuzima means kwenu mnaendana kwa asilimia 25 sikushauri kuwa nar na kama mahusiano yenu hayana u serious wowote jaribu kutafuta wa size yako haijalishi ni miaka mingapi ataficha makucha lakini ipo siku tu atayaonyesha na ndoa moja kwa moja huwa ni mkolezo wa moto wa nyota za watu na ni tendo la kukamilisha nusu ya dini au ibada kwa imani yoyote uliyonayo.

Haijarishi mtaelewana kwa muda gani any second moto huwa unawaka na kila mtu hutizamia nafsi yake na mara nyingi kwa nafasi kubwa kibri chako na ufalme wako au utawala ndio huwa unaleta shida kwa maana asili yako ni simba wa nyika ambaye hahitaji kuwa pinned down na yoyote sasa kwa yeye unakuwa umepamia kwa maana ni Mfalme wa vita na hakubali kushindwa no matter what uwe umemzidi umri,akili,maarifa,au pesa kitakachozidi kushikiria mahusiano yenu ni roho ya huruma na moyo wa imani ulionao.

Yawezekana ukawa na huruma kwa machozi anayokuonyesha na lawama anazotoa lakini nyuma ya shilingi huyu ni nge no matter how utacheza nae atakung'ata tu.

Kukusaliti kwake ni jambo la kawaida na halionei tabu na anaweza kukuumiza roho kwa nafasi kubwa bila kujali na ukitaka kuhoji atakwambia I'm being honest au mimi naongea kwa uwazi na siwezi kuficha nakwambia yaishe lakini katika moyo wake ni kwamba anakwambia ili siku nyingine tena na tena aje akwambie.

Mwenye uwezo wa kuishi na huyu mwenye asili ya maji ya moto ni mtu aliyeshika sana imani ya dini na Bushoke.

na kwa wewe moto wa nyasi dini ni sawa unaweza kuwa nayo lakini kuwa bushoke wenye moto wa mkaa katika milioni 10 labda mmoja.

MTIZAMO WA PILI:
Katika maswala ya ngono na chumbani hakuna mtu kama wewe atakuona ni mtu mwenye kumridhisha sana na hata anaweza kukwambia katika wazinifu wote niliozini nao hakuna kama wewe you are the best unanipatika
Lakini taratibu utaanza kujikuta katika wakati mgumu wa kuendana na tabia zake za wivu kupindukia na kutaka kutawala mahusiano yenu yaani atakutega kila kitu anakusikiliza wewe lakini kiuhalisia utaona bila kujificha kuwa anataka akupande kichwani na usiwe na lakusema ukiwa unaongea nae utaona anakukatisha na kutaka yeye ndio akueleweshe kitu
Ukali na hasira za karibu ni tabia na asili yake no matter how mbele za watu atajionyesha mpole lakini huyu ni short fuse kwako time yoyote bomu inalipuka.
Wakati wewe ni moto mkali zaidi kuliko yeye ni ukali wako ni sawa na gas inayosubiri kiberiti tu ili iweze kulipuka any second akileta udambwi dambwi unaweza kulipuka vibaya na kama unashetani basi hapo hapo hupanda :)
Pia fikra yako ni moja kwa moja utakuwa unamtizama kama kichwa ngumu na mwenye hasira.
Hali ya kuwa wewe anakuchukulia kama mwongo na hupenda kujionyesha.
Hawezi kukuelewa tabia yako ya kupenda kuzungukwa na watu na ataendelea kukudhania kuwa ni mtu mwenye kupenda kujionyesha.
Yeye ni mtu wa kupenda kutawala kuliko kujionyesha na wewe ni mwenye kupenda kujionyesha (kujisifu) na kutawala hata kufaa huyu.
Ingawa kwa ngono mtafurahiana lakini Sex isn’t everything.

 NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !