Mahusiano nyota ya Simba na Mapacha (Leo and Gemini)

Rakims
SIMBA NA MAPACHA


(Leo and Gemini)

Mtizamo unaonyesha wewe ni moto wa mkaa na yeye ni upepo wa pumzi,
mnaendana sana japokuwa kwenye ndoa mnaingia katika mlango wa nane mlango wa kifo na ufufuo.
Mtizamo unaonyesha ni watu mnaweza kuingia haraka kwenye mapenzi au ndoa kwa sababu ni watu mnaweza kuwa na mtizamo mmoja na wenye kupenda mambo mengi yanayoendana.

Hivyo vitu vyenu vingi nyote wawili ni maisha ya kijamii,sherehe,theater(movies & tv-shows) marafiki wengi pamoja na uchangamfu.

Yeye anaonekana anaweza kufungua (joie de vivre) kama ni mtu wa kufuatilia sana series na movies utaelewa namaanisha nini yaani anaweza kukuletea furaha tele ya maisha, mambo yenu ni watu wa kukimbizana na aina mbali mbali za burudani na furaha ya maisha. Nyote mnaonekana kila mmoja ni mwenye kumtafutia mwenzio kuona raha ya maisha kupitia yeye.

Unaonekana ni mtu mwenye kufurahia imagination zake zinazompeleka mbali kimawazo na vile vile uchangamfu wake chumbani na utani/uchokozi unafurahia sana kucheka na kufurahi mkiwa chumbani na ni mtu wa kupata hasira na kuishiwa hamu ya kufanya tendo pale anapojaribu kuweka userious kidogo chumbani.

Yeye anaweza kuwa kichocheo kikubwa cha wewe kuwa na wivu kwake kwa sababu ya njia nyepesi yeye aliyonayo katika kugawa/kusambaza upendo kwa watu tabia yake ya kucheka na kila mtu hukufanya kuamsha hisia zako za wivu .
Unaonekana ni mwenye mihemko na mkali zaidi kuliko yeye. Maisha yenu pamoja yanaonekana ni yenye kusisimua na kukasirisha at the same time,
Lakini mnaweza kukaa kwa furaha na amani ikiwa yeye tu atakuwa muaminifu na kuendelea kubaki hivyo. Vinginevyo tofauti na hapo ni Puuf! hadithi ya mapenzi ya dhati inakuwa imeishia hapo.

Hiyo ni kutokana na wewe asili yako ni kuwa ni mtu mwenye moyo mkubwa na hisia kali na usiyeweza kuvumilia usaliti na mwenye kuweka kitu kwenye roho kwa muda mrefu sana japo ni mwepesi kusamehe ila ni mgumu kusahau.

 NOTE:

Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:

Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !