Mahusiano kinyota Mbuzi na Ng'ombe (Capricorn and Taurus)

Rakims

 MBUZI NA NG'OMBE

(Capricorn and Taurus)



Utangamano
Kwa mtizamo hapa unaonekana wewe na yeye mnaendana kwa asilimia 90 kwa maana ni watu wenye kuendana kiasili ya nyota zenu nyote ni udongo ambapo wewe ni udongo wa pwani na yeye ni mchanga wa fungu hivyo ni watu mnaendana vizuri na pia kindoa mnaingia katika mlango wa 12 yaani ni mlango uliojaa fungo na siri kwako utanufaika sana ukiwa nae na ufuatao ni uchambuzi wenu:

Yeye anaonekana kuvutiwa na makusudio yako katika mahusiano yenu na wewe unafurahia zaidi utulivu wake na upendo kwa ujumla anapokuwa na wewe hujihisi yupo juu na kufarijika zaidi na huvutiwa zaidi na mutikio wako wa mambo yake jinsi unavyokuwa unamakinika nae anajihisi kwako wewe kapata na hata kama bado hajaanza kuonyesha hilo.
Nyote mnashauku sawa za kiardhi na asilia kimwili hisia za pamoja mnakuwa mnaenda vema. Yeye kwako anakuwa kakamatika zaidi kihisia na hujihisi muda wote kwenye mapenzi yeye ni mgeni na wewe ni mwenye kumpokea vema. Pia wivu kati yenu sio tatizo sana kuoneana wivu kwa ziada nyote ni wenye kupenda pesa na ulinzi wa mapenzi hasa kupenda kuwa pamoja pamoja ni watu wenye kutizamia kama wamoja wenye nguvu moja na msiogawanyika mna maelewano ya muda mrefu na mmoja wenu akisema kitu kaelewa basi ni jambo hutoka moyoni nyie wawili ni wenye maridhiano makubwa.

SEHEMU YAKE YA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni shingo na koo ndio maeneo ambayo kuna hisia zake kubwa za kiwazimu ikiwa;- utagusa eneo hilo,kumbusu na kutomasa eneo hilo hata kama umekaa nae basi utampandisha kwa kasi sana hisia zake na hasa ukiwa umekaa karibu nae ukawa unamgusa hapo chochote unachosema kinaingia kwenye akili yake na roho yake moja kwa moja kuhusu wewe.

Ukimbusu eneo hilo vizuri na kumng'ata kichokozi akiwa kalala chali na kwenye koo lake basi utaona maajabu.

Fanya mbinu hii pia itakuongezea umaarufu kwake

Mfanyie massage hii ili kuweza kumfanya siku yake yote ajihisi yupo kwenye raha:

(1)Akiwa kalala kwa mgongo wake muwekee mitetemo kwenye shingo yake karibu na mizunguko ya masikio yake kwa kutumia vidole vyako tumia miondoko ya taratibu sana kwa maana sio punda huyu kama kina fulani huyu anataka vitu sensitive rudia hivyo hadi uone vipele vimesimama kwenye mikono yake. (Be very
gentle kuzunguka sehemu ya pipe za hewa kwenye shingo vinginevyo utamniga).

(2) Kumbuka ni mtu mwenye kupenda zaidi kufanyiwa hivyo akiwa kalala kwa tumbo lake hivyo fanya hivyo hadi kukaribia eneo la muunganiko wa uti wa mgongo lakini usitoke nje ya shingo maana umeme utakatika halafu ataona unamtembezea wadudu.

Ukianza kuona vinyweleo vimesimama na vipele basi jua chini hali si shwari wacha niishie hapa na Ramadhan hii nisije nikafanya mambo magumu masaa yamebaki machache.

Ikiwa utamgusa au kumfanyia manjonjo sehemu za shingo yake basi ni mtu mwenye kupata hisia za kiwazimu na wewe eneo lako kubwa la hisia ni maungio yote ya mwilini ikiwa atakupatia sehemu hizo vizuri kama hamjafunga ndoa basi utataka itokee kesho.

NOTE:
Ikiwa unahitaji kutizamiwa nyota yako na mwenza wako ama mtu unaetaka kuhusiana nae na kujua mtaenda vipi, usisite kuwasiliana nasi:


Gharama sh elfu 5,000

Kwa mawasiliano na huduma:
Wasiliana nasi kupitia:

Email: rakimsspiritual@gmail.com
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp +255 783 930 601

Rakims

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Accept !